Saed Kubenea, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kupitia CHADEMA, ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kushindwa kulipa Sh milioni 9. Kubenea aliyehamia chama cha ACT-Wazalendo, anatakiwa kufika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar es Salaam, Agosti 17, 2020 ambako shauri hilo limefunguliwa. Anayemdai ni Deusdedith Kahangwa ambaye aliyekuwa mwandishi katika gazeti la Kubenea, kupitia Kampuni ya Hali Halisi ...

Mmoja wa wanachama wa CHADEMA aliyekata rufaa kupinga matokeo ya kura za maoni kwenye ubunge Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, ameamua kuondoa rufani yake. Mtia nia huyo, Deusdedith Kahangwa, juzi – Agost 7 aliandika barua (tumeinasa) kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akieleza kuondoa rufani yake kwa sababu za kudorora kwa afya yake. Katika barua hiyo yenye nakala kwa ...

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kimeshindwa kulipa fedha ya siku moja kuendelea na kikao katika hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilichoanza juzi, Agosti 5, 2020 katika hoteli hiyo, kilikuwa cha kumaliza migogoro ya uamuzi kwa watia nia 63 ambao walikata tufaa dhidi ya vikao vya chini. Katika kikao hicho, wajumbe walialikwa kutoka maeneo ...

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Gideon Nasari, bado anapambana kuchomoka katika shauri la rushwa, kutakatisha fedha na matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa ofisini. Shauri hilo ni moja ya mashauri mengine mawili yanayoendelea kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika ofisi zake za Dar es Salaam. Nasari ameongoza NDC kuanzia 2007 ...

Ili Chama cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika Jimbo la Moshi Mjini kunahitajika Umoja na Ushirikiano wa Hali ya Juu na ni lazima Mkakati huo utazamwe kwa Upana bila kuhofu jambo lolote. Kwa sasa Moshi Mjini kuna Mpasuko Mkubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi, Kuna kundi la Matajiri ambao waao ndio wanajiita ‘wenye CCM’ na kuna kundi la Wanyonge ambao wao ...

Baadhi ya wakubwa wa serikali zilizopita, wakiwamo mawaziri, manaibu wao, wakurugenzi wa mashirika, wameanza kuhojiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuhusu mkataba wa kuuza hisa za mgodi wa chuma na makaa ya mawe, Liganga na Mchuchuma. Miongoni mwa vigogo hao ni William Ngeleja, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, wakati mkataba huo unafungwa kati ya Serikali ...

Uchimbaji wa dhahabu katika mgodi wa Buzwagi, ulioko Kahama, Shinyanga nchini Tanzania unatarajiwa kufungwa Machi, 2021. Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa kufungwa kwa mgodi huo kunafuatia kukosekana kwa kiwango cha dhahabu iliyotatajiwa. Imeelezwa kuwa kiwango kijachopatikana sasa ni kidogo mno kiasi cha kushindwa hata kupata mapato ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na mahitaji mengine. Wafanyakazi kupunguzwa Aidha, tumedokezwa zaidi kuwa ...

Inaonekana mzimu wa madiwani waliounga mkono juhudi za Rais John Magufuli unaanza kukitesa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai na mkoa wa Kilimanjaro. Kikundi cha watu kama 200 kilipewa fedha ili tarehe 30 Julai 2020 kiandamane kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Bwana Lengai Ole Sabaya kupinga matokeo kura ya maoni kata ya KIA. Tumeelezwa kuwa katika ...

Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni wamekubaliana kurejesha kwenye Ikulu zao mchakato wa kutandaza bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki. Bomba hilo linaloanzia Hoima, Uganda na kuishia Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, limekwama baada ya kuwepo kwa “vizingiti” ndani ya serikali zao na  hata wawekezaji katika mradi huo. Wawekezaji katika mradi huo mkubwa wa kusafirisha mafuta, ni Total, Tullow ...

Mgombea wa CCM aliyeongoza kura za maoni Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo amekutana kwa siri na masheikh watatu wa BAKWATA akisaka kupata ushawishi wao ili aweze kupitishwa na vikao vya juu vya chama hicho. Katika kikao chao cha siri kilichofanyika  Julai 29, 2020 taarifa zetu zinabainisha kuwa wamekubaliana kwamba kila linalowezekana lifanyike ili jina la mgombea huyo lirejeshwe na ...