Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amewakutanisha maaskofu 71 wa makanisa ya “kiroho” jijini Dar es Salaam akiomba msaada wao ili ashinde ubunge. Maaskofu hao walikutana Alhamisi iliyopita katika hoteli ya Picolo, iliyoko Kawe jijini Dar es Salaam. Taarifa zinaeleza kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa kuomba viongozi hao wa kiimani kupitia makanisa yao kusaidia Gwajima ...

Timu ya kampeni ya mgombea Ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima imeanza kampeni za nyumba kwa nyumba, ikiomba samahani kwa niaba ya mgombea. Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa timu hiyo ya kampeni, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), juzi ilikuwa Kata ya Bunju, ikiongozwa na wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa. Katika kampeni hizo, timu hiyo imekuwa ...

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media Group (CMG), Joseph Kusaga anatuhumiwa kufuja fedha za kampuni, matumizi mabaya ya uongozi na dhuluma kwa wanahisa wengine, zikiwemo za marehemu baba yake. Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa Joseph, maarufu kwa jina la Joe, amekuwa akitumia fedha zinazopatikana kupitia Clouds FM, kuanzisha biashara binafsi, kukwapua mali, hasa nyumba na mashamba ambayo yalinunuliwa kwa fedha za ...

Vitengo vya Usalama katika baadhi nchi na taasisi za kimataifa, vimetuma watu wao kufuatilia kwa karibu mchakato mzima wa kampeni za Uchaguzi wa Tanzania. Vyanzo vyetu vinaeleza kuwa maofisa wa nchi na taasisi hizo tayari wako nchini wakichunguza mienendo ya viongozi wa vyama, hasa wagombea urais, wakati wa kampeni. Imebainika kuwa miongoni mwa maofisa hao ni mawakili kutoka Mahakama ya ...

Makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao majina yao hayakupitishwa kugombea ubunge, wamewasilisha barua kuomba sababu za kukatwa. Wawili kati ya hao watatu, licha ya kuongoza katika kura za maoni, majina yao yalikatwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), hivyo kuenguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho tawala kwenye uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba 28 l, mwaka huu, 2020. Taarifa ...

Makao Makuu ya Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania, mchana huu yamevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni maofisa wa Serikali na kuondoka na baadhi maofisa wake. Taarifa zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa maofisa hao huenda wanatoka moja ya taasisi nyeti za Serikali. Maofisa hao wameondoka na viongozi wanne wa Total wakiwa wamefungwa pingu na kupandishwa ndani ya magari mawili yaliyowasili ...

Mbio za kuwania urais wa Tanzania kwa Tundu Lissu, huenda zikafikia ukingoni siku chache  baada ya kukabidhi fomu zake Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC). Lissu alipitishwa na chama chake, CHADEMA kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi wa mwaka huu, 2020 uliopangwa kufanyika Oktoba 28. Taarifa za uchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa CCM, Serikali (kwa kutumia Idara ya Usalama wa Taifa) na baadhi ...

Atleast seven Tanzania political and government leaders, two in the incumbent government – have been found to own properties (houses) in Johannesburg and Durban, South Africa. Investigations demonstrate that the kleptocrats have favoured real estate in South Africa cities as a means for hiding their money, believed to be ill gotten, especially from corruption and money laundering. The spotted officials ...

Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga anashikiliwa na kikosi kazi cha Serikali kutoka Makao Makuu Dar, kinachohusika na kukusanya madeni. Taarifa za uhakika zinasema Kalanga amekamatwa leo majira ya jioni nje ya ofisi za NMB na askari wa Takukuru na baadaye kupelekwa ofisi za TAKUKURU mkoa. Akiwa njiani inadaiwa alikuwa akilalamika kwamba Mdhamini wake wa Mkopo huo Ndugu Kadogoo amemkimbia ...

Kosa moja la kiufundi linaloweza kufanywa na Kamati Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na kupelekea jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro ni kumpitisha mgombea ubunge aliyegushi shahada yake ya sheria. Huyu ni Habib Mruma aliyeshika nafasi ya tatu ambaye Baraza la Seneti la chuo Kikuu Mzumbe katika mkutano wake wa 67 uliofanyika tarehe 25 Novemba ...