Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima amethibitika kugawa Sh. 20,000,000 kwa kila kata.
Uchunguzi wetu umebaini kwamba mgombea huyo amekuwa akigawa kiasi hicho cha fedha kila anakopita kufanya kampeni.
Jana katika Kata ya Msasani Kisiwani, Kinondoni, Gwajima akiwa katika kampeni alikutana na viongozi wa vikundi vya vijana vya uhamasishaji na ujasiriamali na kuwakabidhi Sh. 20, 000,000.
Alisema, “Hii siyo rushwa, mimi nawawezesha tu muweze kujikwamua kiuchumi.”
Askofu Gwajima amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wagombea wenzake kwamba anatembeza rushwa ili kujihakikishia ushindi wa jimbo hilo ambalo hadi Bunge linavunjwa lilikuwa likiongozwa na Halima Mzee, kutoka CHADEMA.
Ushindani katika Jimbo la Kawe umekuwa mkubwa baina ya Gwajima na Mdee huku kila mmoja akionekana kuwa na nguvu inayoweza kupelekea atangazwe mshindi.
Leave a Reply