Dkt. Bashiru, usidhani umefika! Unaliwa timing tu

Taarifa tulizo nazo zinaonyesha Bwana Mkubwa anakulia timing tu, kuna mtu anaandaliwa kuishika nafasi yako wakati wowote baada ya Uchaguzi.

Huyu ni naibu wako, Rodrick Mpogolo ambaye kina Polepole na Msigwa wanapambana kila uchao kuhakikisha anakuwa SG wa CCM na wewe ukachinjiwe baharini. Kimsingi, Polepole pia anaitamani nafasi yako.

Huenda hujasoma alama za nyakati, sisi tunakudokeza mapema. Hiki ndo chanzo cha Mpogolo kuwa Meneja wa Kampeni kwa mwaka huu 2020 na hakuna aliyetarajia hata siku moja kuwa angepewa nafasi hii nyeti.

Kimsingi, kuna mkakati aidha usukumizwe kwenye ubunge au uteuliwe ubalozi. Hapo genge la Polepole na watu wake wa Iringa litakuwa limefanikiwa kukumaliza.

Wanatumia udhaifu wa Bwana mkubwa kufuatia kutofautiana kwako naye kwenye uteuzi wa wagombea ubunge na ukatwaji wa baadhi ya majina wakati wa mchakato wa kupitisha wagombea. Kukusaidia, fuatilia kupitia vyanzo vyako utabaini kuwa Polepole na wenzake walishavuta ‘mzigo’ toka kwa baadhi ya wagombea