Hawa ndio waliokopa kwenye mabeki na kukimbia Tanzania

Waliokopa hela katika mabenki na kukimbia ni pamoja na bwana Shabir Shamshudin Abji aliyekuwa anamiliki hisa za New Africa Hotel. Wengine ni Ramesh Nandrabhai Patel aliyekuwa mbia wa Bank M na mmiliki wa Auto Mech, Mzee Baghdela anayemiliki vituo vya mafuta kikiwemo cha Puma (ya pale Posta karibu na Serena Hotel) na Mmiliki wa Star Minerals (Tanzania) aitwaye Otto Mosha.

Walikopa wapi?

Bank M, TIB (ya Mlimani City) na Amana Bank.

Kuna kesi zipo kwa DCI tangu akiwepo Boaz ila Boaz alikuwa mtu wa karibu na Ramesh Nandrabhai Patel hivyo akawa anazizima zisiendelee. Baada ya Boaz kuondolewa ndio zile kesi zikaenda mahakamani.

Lobbyist anayetumika kuhonga ofisi ya DCI ili kesi zisiende mbali zaidi ni mtoto wa Ramesh aitwaye Heena Ramesh Patel.

Na mfano baada ya Bank M kufilisika ilirithiwa na Azania Bank. Mali za wadeni sugu wa mikopo chechefu zikapaswa kuuzwa katika mnada na kampuni ya udalali iitwayo Mark Auctioneers ila dalali huyu akawa anakwama kwasababu wadeni wakawa wanahonga kuvuruga minada.

Kuna wakati Ramesh Nandrabhai Patel alikamatwa. Akawekwa ndani gereza la Keko akafunguliwa mashitaka ya utakatishaji fedha. Akafanya plea bargaining, akalipa fidia na kutoka. Yupo mtaani sasa hivi.

Ramesh Patel anajitambulisha kama mtu wa karibu wa Mzee Kinana.

Waliokopa kupitia Bank M wengi hela zao wamezihamishia nchini Kenya kwa kufungua Benki mpya iitwayo M-Oriental Bank ambayo ni pacha wa Bank M.

Aliyekuwa m-NEC (CCM) kupitia mkoa wa Mara ndugu Paul Henry Kirigini katumika sana kufikisha rushwa kwa maofisa wa BOT ili wabia wa Bank M waliokopa mikopo chechefu wasichukuliwe hatua. Rushwa zilikuwa zinatolewa na Shabir Abji na Ramesh Patel na mpokea hongo ni aliyekuwa Naibu Gavana, Dkt. Bernard Kibesse.

Ikumbukwe kuwa waliokuwa wabia wa Bank M ndio walioifilisi TiB ya Mlimani City, Bank M yenyewe na baadhi hata Amana Bank walipiga hela kwa mtindo wa mikopo chechefu.

Ili TiB ya Mlimani City iweze kurejesha hela yake ilifanikiwa kuuza kwa mnada assets za Auto Mech kwa ASAS.

Aliyesaidia TiB kutoa mikopo chechefu ni Erick Benedict Hamis aliyewahi kuwa DG wa TPA na sasa ni DG wa Shirika la Meli. Na ndio ilikuwa sababu ya kuondoka TiB. Alikuwa miongoni mwa wakurugenzi waliohusika kwa ukaribu na masuala ya mikopo pale TiB (ripoti za uchunguzi zipo Ofisi ya Rais).

Kuna kampuni inaitwa Grant Thornton Tanzania ambayo inamilikiwa na Ketan Shah. Huyu aliwahi kuwa mbia wa KPMG hapa Tanzania. Shah ndio alikuwa CFO wa Bank M. Ndiye aliyetoa tathmini ya madhara ya mikopo chechefu katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Bank M. Hakuwafurahisha wakubwa, akafukuzwa kazi siku iliyofuata. Huyu ni shahidi mzuri kwa serikali. Anawindwa sana na Ramesh Nandrabhai Patel kwa kuhofiwa atatoa siri za namna Bank M ilivyokuwa inaendeshwa.

Katiba wabia wa Bank M, yumo kada mkongwe wa CCM, Christopher Mwita Gachuma.

Rais Samia hivi karibuni amtaja mtu kukopa katika benki 15. Sawa, ila katika hizo benki 15 ni benki 3 tu ndio zilikuwa na hali mbaya. Bank M, Amana Bank na TiB ya Mlimani City.

Bwana Otto Mosha amefungua kesi mahakama kuu kupinga mali zake kupigwa mnada kwasababu overdraft ya mkopo wake imefanywa kihuni kwa Ramesh Patel na aliyekuwa CEO wa Bank M, Ndg. Sanjeev Kumar kufoji saini zake na baadhi ya nyaraka kisha wakakwapua mamilioni ya hela.

Sanjeev Kumar kwa sasa inasemekana amekimbilia Kenya na anadaiwa kutoroka nchini kwa msaada wa wakili wake aitwaye Hudson Ndusyepo.