WATUMISHI WA NHIF HATUMTAKI MKURUGENZI MKUUWA NDG. BERNARD KONGA KUTOKANA NA UONGOZI MBOVU ULIOJAA UPENDELEO NA UONEVU KWA WATUMISHI

Tunaomba Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan na Ofisi ya Rais pamoja na wasaidizi wako Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein A. Kattanga, Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mathew Mwaimu, Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji wa Rufani Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Ndg Juma Muhimbi mpokee kilio chetu. Watumishi wa NHIF hatuna morali ya kazi kutokana na uongozi mbaya wa Mkurugenzi Mkuu Ndg. Bernard Konga uliojaa upendeleo, uonevu na uvunjaji wa Sheria za utumishi wa umma na maadili ya utumishi wa umma. Tafadhali pokeeni tuhuma zenye ushahidi zinazoharibu morali ya NHIF kwa watumishi kama ifuatavyo;

  • Mkurugenzi Mkuu alishiriki 100% kuishawishi Bodi kumpitisha Mkurugezni wa Rasilimali Watu Ndg. Charles Lengeju ambaye hakushinda usaili uliotangazwa mwaka 2016 na hakuwa na sifa ya Digrii ya Uzamiri. Uchunguzi ulifanyika ikabainika kwamba Mkurugenzi Mkuu ndiye alisimamia uvunjifu wa utaratibu wa usaili na uteuzi wa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala na kuishawishi Bodi iliridhie uvunjifu wa taratibu za usaili na uteuzi wakati Watanzania waliofaulu wakiachwa. Baada ya uchunguzi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala ameshushwa Cheo na kuwa Afisa Mwandamizi na kuhamishiwa Ofisi ya NHIF Temeke. Upendeleo huu umeleta madhara makubwa kwa Watumishi kutokana na Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala kufanya kazi kwa mashinikizo ya Mkurugenzi Mkuu.Watumishi tunajiuliza na kugawanyika kwamba kama uvunjifu huu ulisimamiwa na Mkurugenzi Mkuu yeye kwanini hajawajibishwa kwa kutosimamia NHIF kwa mujibu wa Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma.
  • Ofisi ya Rasilimali Watu haina Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala tangu mwezi Machi, 2022. Sheria za Utumishi zinaelekeza nafasi ikiwa wazi itangazwe ndani ya NHIF au kwa Watanzania wote ili waombe. Mpaka sasa nafasi inakaimiwa, anayekaimu ni Meneja wa Rasilimali Watu Ndg. Lameck Kabeho ambaye naye aliletwa kutoka Taasisi ya Madini hivyo anafanya kazi kwa maelekezo na mashinikizo ya Mkurugenzi Mkuu. Upendeleo unaotaka kufanyika ili Meneja huyu awe Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utaratibu unazigi kutugawa na kuvunja morali ya kufanya kazi.
  • Taratibu za ajira za utumishi wa umma zinaelekeza nafasi zilizo wazi zijazwe na watu wenye sifa. Nafasi ya Meneja wa Madai imekuwa inakaimiwa na Mfamasia Ndg. Cosmas Mogasa ambaye hana sifa za kuwa Meneja kwani hana Digrii ya Uzamiri. Mkurugenzi Mkuu akiwa anafahamu ni uvun jivu wa taratibu za ajira alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu ampe nafasi hiyo na sasa ameambiwa asome Digrii ya Uzamiri ili athibitishwe kuwa Meneja kamili. Ndani ya NHIF wako Watumishi wenye sifa ya kuwa Meneja Madai lakini hawajapewa haki ya kuomba nafasi hiyo na kuteuliwa licha ya kukidhi sifa zaote. Upendeleo huu unatugawa wafanyakazi wa NHIF hasa wale wenye sifa.
  • Mwaka 2018 zilitangazwa nafasi za Mameneja wa Mikoa ya Mtwara, Ilala, Kigoma na Songwe. Pamoja na sifa zingine waombaji walipaswa kuwa na Digrii ya Uazmiri. Mkurugenzi Mkuu aliishinikiza Kurugenzi ya Rasilimali watu kuvunja masharti ya Tangazo la nafasi hizo na kuwaita watumishi wote lengo likiwa ni kuwapendelea Watumishi waliokuwa wanakaimu nafasi hizo kwa mikoa ambayo haikuwa na Mameneja na wote wakiwa hawana Digrii za Uzamiri. Mwenyekiti wa Usaili ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TRA alibaini vitendo hivyo na kuwafukuza wote waliokuwa hawana sifa ya Digrii ya Uzamiri. Kibaya zaidi wakati wa kupeleka majina ya washindi wa nafasi za Mameneja wa Mikoa kwenye Kikao cha Bodi ili wateuliwe, Mkurugenzi Mkuu alishimshinikiza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kwenye orodha ya majina ya washindi awaongezee Ndg. Kuhunga Msambichaka kama Meneja wa Vitambulisho na Ndg. Victor Wanzagi Meneja wa Mipango licha ya nafasi hizi kutotangazwa ili Watumishi wenye sifa waombe. Hivyo Maneja hawa wawili walipendelewa kinyume na taratibu za uteuzi. Watumishi tunajiuliza kwamba kama uvunjifu huu ulisimamiwa na Mkurugenzi Mkuu yeye kwanini hajawajibishwa licha ya Taasisi za Serikali zilizo chini ya Rais kufahamishwa na kufanya uchunguzi na kuthibitisha upendeleo na uvujifu wa taratibu za ajira.
  • Mkurugenzi Mkuu amekuwa anashirkiana na Meneja wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Stephen Shauritanga kugawana fadha za safari ambazo meneja huyo na baadhi wa Watumishi wa Ofisi ya Mkoa walikuwa wanagawana fedha lakini hawasafiri bali wanagbaki Ofisini. Licha ya Meneja wa Mkoa kujihusisha na wizi wa fedha za Serikali kwa zaidi ya miaka 4 ambapo zaidi ya Tsh. 200,000,000 zilikuwa zinagawanwa na Mkurugenzi Mkuu akifahamu hawakuwahi kuchukuliwa hatua zozote zaidi ya Mkurugenzi Mkuu kumlinda Meneja wa Mkoa wa Dodoma. Hata hivyo, wizi huu uliripotiwa TAKUKURU na uchunguzi ukafanyika na kuthibitishwa Meneja wa Mkoa pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Dodoma walikuwa wanagawana fedha ha hawaendi kwenye kazi za nje kwa mujibu wa maadiko. Meneja huyo baada ya kukiri TAKUKURU na kukubali yeye na baadhi ya Watumishi kurudisha fedha hizo, Mkurugenzi Mkuu hakuwahi kumchukulia hatua yoyote licha ya wizi huo kuthibitishwa na TAKUKURU. Ikiwa watumishi waliothibitishwa kuiba fadha zaq shirika walifukuzwa mara moja kwanini Mkurugenzi Mkuu wengine anawachukulia hatua na wengine wanabaki Ofisini licha ya wahusika kukiri. Tunaona vitendo hivi ni kinyume na Sheria za utumishi pamoja na Maadili ya Viongozi wa UMMA.
  • Nafasi ya Mkurugezi wa Fedha ilibaki wazi kwa zaidi ya Mwaka sasa baada ya Mkurugenzi kufukuzwa kazi kwa tuhuma za wizi wa fedha za Mradi wa KFW wa Mama Wajawazito. Nafasi hiyo imekuwa ikikaimiwa na Meneja wa Fedha Ndg. Latens Wella kwa mwaka lakini mpaka sasa hajathibitishwa kazini. Kilichofanyika, Mkurugenzi Mkuu kwa kushirikiana na Meneja wa Rasilimali Watu anayekaimu Ndg. Lameck Kabeho wakijua wanavunja Sheria za Utumishi za Ajira na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma waliwaita kimya kimya baadhi ya Watumishi wa Mfuko bila kutangaza nafasi hiyo ili wafanye kama kukamilisha taratifu ionekane baadhi ya Watumishi walishirikishwa ili wampendelee Mtu wanayemtaka awe Mkurugenzi wa Fedha. Kuficha utaratibu wa kumpata Mkurugenzi wa Fedha na kuwaita baadhi ya watumishi bila kutangaz nafasi hiyo ndani au kwa Umma umelenga kupendelea. Taasisi inaendeshwa kwa upendeleo na namna anavyojisikia kufanya Mkurugenzi Mkuu. Kwa utaratibu huu tunaona tumechoka kuongozwa na Kiongozi asiyesimamia Sheria na Miongozo ya Utumishi.
  • Mwezi Julai, 2022 Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilitangaza posho kwa Wakurugenzi wa Taasisi na Maofisa na Wasio Maafisa. Posho zilizotangazwa kwa Wakurugezi ikiwepo NHIF ilikuwa ni Tsh. 250,000, wakati Mameneja ni Tsh. 220,000 kwa majiji na miji mikubwa. Hata hivyo, katika Waraka wa NHIF uliotolewa Julai 15, 2022 Mameneja waliokuwa awanalipwa Tsh. 250,000 walipunguzwa posho na kuwa Tsh. 220,000 kwa mujibu wa Waraka wa Ofisi ya Rais. Hata hivyo, posho ya Mkurugenzi Mkuu anayelipwa Tsh. 600,000 ameiacha ibaki hivyo wakati posho ya Wakurugenzi wanaolipwa Tsh. 300,000 nayo imebaki hiyo hiyo. Upendeleo huu wa kupunguza posho za Mameneja zinawa Tsh. 220,000 lakini za kwako zikabaki kama zilivyo ni upendeleo kwamba Mkurugenzi Mkuu aliona aendelee kujipendelea yeye na awaongeze na Wakurugenzi jambo ambalo ni kinyume na Waraka wa Ofisi ya Rais. Kama waliamua kuendelea kujilipa posho za Tsh. 600,000 kwa Mkurugenzi Mkuu na Tsh. 300,000 kwa Wakurugenzi hata Mameneja na Maafisa wangeendelea na posho za awali. Vitendo hivi vya upendeleo vinatugawa sana Watumishi.
  • Mhe. Rais na wasaidizi wako, kwavile NHIF ina whistleblowing policy inayoruhusu Watumishi kutoa taarifa mbalimbali ndani ndani nan je ya Taasisi ili zifanyiwe kazi, ninaomba kutoa taarifa hizi za kweli ambazo baadhi zimeshafanyiwa kazi na kuthibitishwa na nyingine bado. Tunaomba Mh. Rais ufanye maamuzi juu ya Kiongozi huyu ili kunusuru mgawanyiko uliopo baina ya Watumishi na kurudisha morali ya kufanya kazi kwa kujituma.