Kampuni ya Mwananchi kukwama zaidi. Nanai ang’atuka

Kushuka kwa mapato ya mauzo ya gazeti la Mwananchi na kuzuiwa kwa matangazo mengi toka taasisi na mashirika ya umma na serikali kunaongeza uchungu katika mlolongo wa changamoto za ustawi wa gazeti hilo kwa sasa.

Kwa muda mrefu sasa, gazeti hilo limekuwa likichechemea kiuchumi huku taarifa za ndani zikionyesha kuwa limeanza kuelemewa na madeni yanayotokana na gharama za uendeshaji, hasa uchapaji. Gharama kubwa katika uchapaji zinahusisha ununuzi wa karatasi, wino, umeme na usafirishaji. Pia zipo gharama za uendeshaji wa ofisi.

Ofisi za mikoa, kanda zafungwa

Kutoka na mdororo wa uchumi, Mwananchi imelazimika kufunga baadhi ya ofisi zake mikoani na kanda. Tayari kanda za Tanga, Moshi, Mtwara, zimefungwa.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa mdororo huo pamoja na kuchangiwa na kukosekana kwa matangazo, uchakataji wa habari za gazeti hilo kwa sasa umekosa mvuto kwa wasomaji wake, ambao wengi wanaona kama limekosa habari za “kusaka na kuchambua.”

Gazeti hilo lililokuwa likiongoza kwa kuingiza nakala sokoni, sasa linaelemewa na mabaki ya magazeti yanayoshindwa kuuzika.

Kushuka kwa mauzo ya gazeti na maslahi ya wafanyakazi

Tangu mwanzo wa mwaka 2020, mauzo ya gazeti yamekuwa yakishuka kwa kasi ya ajabu. Mwananchi iliyokuwa ikichapa nakala 55,000 hadi 60,000, hivi sasa inachapisha nakala 15,000 au zaidi kidogo na bado kuna mabaki.

Taarifa zinaeleza kuwa kutokana na kushuka kwa mapato, hivi sasa waandishi na wafanyakazi wa idara nyingine waliopo Mwnanchi, tarehe za kulipa mishahara zimesogezwa mbele na hata kuingia mwezi mwingine.

Wakati wa neema, Mwananchi ilikiwa ikiwalipa wafanyakazi wake mishahara tarehe 24 au 25 ya mwezi husika, lakini sasa wanalipa hadi tarehe 7 ya mwezi unaofuata.

Francis Nanai na kulazimisha habari za kuchapwa

Chanzo chetu kinabainisha kuwa aliyekuwa kiongozi wake mkuu, Francis Nanai alikuwa akilazimisha habari za kuibeba serikali, na CCM, akiweka mazingira ya kwenda kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho tawala Jimbo la  Busega.

Nanai alitangaza kuachia ngazi Julai 30, 2020. Nafasi kiongozi wa gazeti hilo sasa inakaimiwa na Bakari Machumu, ambaye ni Mhariri Mtendaji.

Kesi zaliandama gazeti

Aidha, gazeti hilo la kila siku linalomilikiwa na Nation Media ya Kenya linakabiliwa na kesi tano katika taasisi za mgogoro ya kikazi na mahakama baada ya kuwafukuza na kukatiza mikataba wafanyakazi wake. Miongoni mwa wafanyakazi hao ni waandishi wawili: Ibrahim Yamola na Neville Meena.

Julai 6, 2020

Mwishoni mwa wiki iliyopita walitangaziwa kufunga ofisi zao zote za mikoa isipokuwa Dodoma. Mwisho wa ofisi za mikoa kufanya kazi ni mwezi huu. Samani za ofisi za mikoani zimetakiwa kurejeshwa Dar. Watendaji waliokuwa mikoani wametakiwa kurudi Dar auwatrakaopenda kubaki huko basi wakubali kuwa correspondents.

Ofisi ya Zanzibar kodi inaisha mwezi Juli, Mkuu wa Bureau amembiwa arudi Dar.

Mwandishi aliyefanya kazi nao kwa miaka 20 amefukuzwa kwa kupigiwa simu tu, ni Salma Said wa Zanzibar.