Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga agombana na Diwani. Ushoga wahusishwa

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga, Salehe Mkwizu, ameingia katika kashfa kubwa baada ya kupigana na Diwani wa Kata ya Kighare, Innocent Msemo kiini kikitajwa kuwa masuala ya ushoga.

Taarifa zinadai kuwa tukio hilo la aibu na kufedhehesha lilitokea tarehe 21,2022 katika baa mashuhuri ya MBC katika mji mdogo wa Mwanga, na tayari mwenyekiti huyo ametakiwa kujisalimisha polisi na kusalimisha pia bastola yake anayomiliki kihalali.

Walioshuhudia tukio hilo waliliambia Imevuja kuwa siku hiyo, mwenyekiti na Diwani huyo walikuwa wakipata vinywaji na Mwenyekiti inadaiwa alimtamkia mwenzake maneno ambayo ndio yalikuwa kiini cha ugomvi.

“Inavyoelezwa ni kuwa walipokaribia kuondoka mwenyekiti alimwambia Diwani Msemo kuwa siku hiyo hataenda “kumfanya” kwa kuwa sio zamu yake na kwamba ana mgeni ambaye ni mwanamke aliyemtembelea.

Inadaiwa kuwa Diwani huyo alihamaki na kumuuliza mwenyekiti “umesemaje”?, na mwenyekiti inadaiwa aliyarudia maneno hayo jambo ambalo lilimfanya Diwani huyo amrukie na kuanza kupigana kabla ya kuamuliwa na walinzi na wateja waliokuwepo hapo.

Mwenyekiti na Diwani huyo ni maswahiba wa karibu na wana maelewano ya karibu kiasi kwamba huvaa nguo zinazofanana kimtindo.

Katika purukushani hizo mwenyekiti huyo alidondosha kitabu cha umiliki wa silaha na haikufahamika kama alikuwa nayo wakati huo ama la, lakini kitabu hicho kiko mikononi mwa Polisi ambao wamemtaka ajisalimishe na asalimishe silaha yake wakati tukio hilo likichunguzwa.

Taarifa zinasema huenda Madiwani wa Halmashauri hiyo wakaibua jambo hilo kesho tarehe 29 Septemba 2022 wakati Baraza la Madiwani litakapoketi kutokana na kuchukizwa na tukio hilo ambalo limekuwa gumzo na limesambaa katika viunga vyote vya wilaya ya Mwanga.