Mkuu wa Nchi anafariki akiwa madarakani… Huyu ndio Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa hili. Sasa anafariki akiwa madarakani. Hiki kiti ndio cha juu zaidi kwenye kila nchi. Hiki kiti ndio nchi yenyewe. Yaani Rais ndio nchi yenyewe (Usiopumbazwe na protokali za kisiasa). Katibu Mkuu Kiongozi anaaga Dunia akiwa kwenye kiti chake. Kwa wasiofahamu, huu wadhifa ni mkubwa sana kwenye utawala ...

Wazalendo wameamua kuyaanika haya. Vyombo vya usalama vifuatilie tuhuma hizi na kuzifanyia kazi, vinginevyo Tanzania chini ya Samia haitakuwa katika mikono salama. Hatua zikianza kuchukuliwa, itatupa matumaini mapya. ...

Inashangaza sana! Mtumishi wa Umma kuvimbishia kifua viongozi wote wa Taifa hili, kisa tu yeye ni Daktari wa Rais. Profesa Mchembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Daktari wa Rais na aliyepata kuwa Mkuu wa Hospitali ya Emilius Mzena inayoendeshwa na Idara ya Usalama wa Taifa anaonekana kuwa na nguvu kuliko kiongozi yeyote mwingine nchini ukiachia Rais Dkt. John Pombe ...

Chanzo chetu cha uhakika kinabainisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Bara, Komredi Rodrick Mpogolo ndiye anatarajiwa kuwa mrithi wa Dkt. Bashiru Ally katika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Disemba 13, 2016 Halmashauri Kuu ya CCM ilimteua Mpogolo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara akichukua nafasi ya Rajab Luhwavi aliyeteuliwa kuwa Balozi. Amewahi kuwa Mkuu ...

WAWEKEZAJI na matajiri wa viwanda katika nchi kadhaa duniani, familia ya Jamal Hassan Abdullah Alawadhi ya Kuwait, wamekumbana na mkwamo wa kuanzisha kiwanda cha dawa nchini Tanzania baada ya kuleta nchini kiasi cha Euro 150,000,000 ambazo ni takribani Shilingi za kitanzania bilioni 425, ambazo bado zinadaiwa kushikiliwa na serikali kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Chanzo Familia ya matajiri hao ...

Ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejiandaa kulinda usalama wa Wabunge wa viti maalum wa CHADEMA dhidi ya tuhuma na hata vurugu wanazoweza kufanyiwa na yeyote. Msimamo huo umetolewa faragha jana na Spika Job Ndugai kwa wabunge hao aliokutana nao ofisini kwake Dodoma. Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa hata kama wabunge hao wataitwa na chama ...

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuomba Mufti wa Zanzibar, Salehe Kaab, kukutana na Maalim Seif Shariff Hamad ili kumfikishia ‘ujumbe wake’. Taarifa zilizotufikia jioni ya leo zinaeleza kuwa Mufti Kaab tayari ameomba miadi ya kukutana na Maalim Seif sikiu ya Jumapili, Novemba 8, 2020 Chanzo cha IMEVUJA kimeeleza kwamba Mufti Kaab amebeba ujumbe wa Rais Dkt. Mwinyi unaoomba ...

Vyanzo vyetu vya uhakika vinadokeza kuwa huduma ya Mawasiliano ya Mitandao ya kijamii zitaanza kurejea kuanzia kesho Novemba 7. Mojawapo ya vyanzo vyetu kimetudokeza kuwa watoa huduma (ISP) wameshaanza kupewa maelekezo kuanzia leo warejeshe huduma hiyo ili wananchi wapate kuwasiliana bila vikwazo kama ilivyokuwa hadi tunaandika taarifa hii. Mitandao mingi ya kijamii ilizuiliwa (blocked) kuanzia Oktoba 27, 2020 ikiwa ni ...

Viongozi wa CHADEMA, Freeman A. Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Taifa na aliyekuwa Mbunge na mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless J. Lema walihamishiwa kituo cha Mlandizi mkoani Pwani juzi. Haijafahamika mara moja lengo la kuwatenganisha na wenzao na sababu hasa za kupelekwa Pwani ingawa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi kinabainisha kuwa lengo lilikuwa ni ...

Polisi wamerandaranda sehemu alipo Lissu ili wamkamate upya. Taarifa kutoka chanzo cha uhakika zinadai makachero na Polisi wametanda kila sehemu wakisubiri atoke tu na kumtia mbaroni baada ya kubaini kuwa jana walikosea kumkamata eneo ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Kimataifa ni makosa. Lissu akikamatwa, inasemekana atafunguliwa mashtaka ya uhaini (si ugaidi) na mkakati ni kuhakikisha anabaki kizuizini kwa muda ...