Prof. Mabula Daudi Mchembe anapobinafsisha Afya ya Rais!

Inashangaza sana! Mtumishi wa Umma kuvimbishia kifua viongozi wote wa Taifa hili, kisa tu yeye ni Daktari wa Rais. Profesa Mchembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Daktari wa Rais na aliyepata kuwa Mkuu wa Hospitali ya Emilius Mzena inayoendeshwa na Idara ya Usalama wa Taifa anaonekana kuwa na nguvu kuliko kiongozi yeyote mwingine nchini ukiachia Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye kwa sasa yuko katika hali tete akipigania uhai wake!

Usiri na vigugumizi vya viongozi katika kuzungumzia afya ya Rais unatokana na Profesa Mabula Daudi Mchembe, ambaye kwa ukaribu wake na Rais na udugu wa kifamilia ameamua hakuna kiongozi yeyote kumuona Rais hivi sasa na wala hakuna maelezo anayotoa kuhusu hali ya afya ya Rais.

Vyanzo vyetu vinatuarifu kuwa tangu Rais alipolazwa katika hospitali ya Mzena Kijitonyama hakuna kiongozi aliyefika kumuona kutokana na makatazo na ubabe wa Profesa Mchembe, hata Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye kimsingi ndiye mwenye hospitali na pia Profesa Mchembe ni mtumishi wake katika Idara, amefika tu hospitali lakini hajaweza kumuona Rais. Inashangaza sana!

Profesa Mchembe ambae unaweza kusema ameamua kubinafsisha afya ya Rais kwa kuwa tangu amelazwa amekishajichotea mamilioni ya fedha akidai ni za madawa, vifaa na nyenzo nyingine muhimu katika kumtibu Rais, zaidi ya shilingi milioni 800 amekwishajitwalia tangu Rais amelazwa hapo, ndiyo sababu hataki mtu yeyote kuingia katika chumba alimolazwa Rais, ni dili kwake!

Inafahamika kuwa Rais alikolazwa kuna vitanda viwili, cha Rais mwenyewe na cha Profesa Mchembe ambae yuko hapo masaa yote kumhudumia mgonjwa, zaidi yake wanaoingia ndani ya chumba hicho ni wawili tu, Muuguzi anayehusika na huduma kwa mgonjwa kwa kuwa hali ya mgonjwa hivi sasa kila kitu ni hapo hapo, hajielewi na hajitambui. Na mwingine anayeingia ni muuguzi anayehusika na kubadilisha mitungi ya Oksijeni kwa mgonjwa pamoja na mashine ya kupumulia (ventilator). Mgonjwa hajielewi, hajitambui. Wengine wa hospitalini hapo wanatumia msemo, Rais ni clinically dead…

Kwa kufikia hapo, ilipaswa mamlaka zaidi ya Profesa Mchembe kwa vipengele kadhaa vya Katiba kujua hali halisi ya Rais, ili Makamu wa Rais awe ni Kaimu Rais wakati Rais anapata matibabu na iwapo itakuwa hawezi tena kurejea katika hali yake ya kuweza kutekeleza majukumu basi vifungu vinavyompa Makamu wa Rais mamlaka kamili ya Urais vitumike lakini ubabe wa mtu mmoja umesababisha hivi sasa hakuna ajuaye, tutaendelea hivi mpaka lini?

Ubabe wa mtu mmoja unapaswa kukomeshwa. Ni nani wako nyuma ya Profesa Mchembe? Ubabe huu anaouonyesha nani anamkingia kifua? Mamilioni yanayotoka (anayolipwa Profesa Mchembe bila taratibu za matumizi ya umma) nani anaidhinisha? Kwanini viongozi hawaruhusiwi kuingia kumuona Rais? Hali hii mpaka lini?

Afya ya Rais sio mzaha, isiwe dili la watu kujibinafsisha. Kwanini Profesa Mchembe anaachiwa hivi?

Vyema mamlaka za juu yake, yeye ni Katibu Mkuu kuna Waziri mwenye dhamana naye, yeye ni Daktari katika Hospitali ya Mzena, kuna Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, washughulike naye!?

Vinginevyo rasilimali za nchi zitaendelea kutafunwa kwa jina la ‘mgonjwa’ ambaye kikatiba alikwisha poteza sifa za kuwa Rais kitambo!

Tutafakari! Tuchukue hatua!