CCM Moshi Mjini kwadaiwa kuwa na mpasuko mkubwa

Ili Chama cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika Jimbo la Moshi Mjini kunahitajika Umoja na Ushirikiano wa Hali ya Juu na ni lazima Mkakati huo utazamwe kwa Upana bila kuhofu jambo lolote.

Kwa sasa Moshi Mjini kuna Mpasuko Mkubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi, Kuna kundi la Matajiri ambao waao ndio wanajiita ‘wenye CCM’ na kuna kundi la Wanyonge ambao wao wanajiita Wanachama wa kweli wa CCM.

Haya Makundi mawili ndiyo yanaenda kuupa ushindi Upinzani kwa mara nyingine pale Moshi Mjini kama tu CCM haitotatua hili tatizo.

Viongozi wa CCM Mkoa hawana uwezo wa kusema chochote mbele ya kundi hili la Matajiri linaloongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, pamoja na Mtia nia wa Moshi Mjini ndugu Ibrahim Shayo. Kundi la Matajiri linahitaji watu wao wapitishwe kwenye vikao vya kamati za Siasa kata na Wilaya hata kama walishindwa kwenye kura za Maoni na hata kama hawana sifa kwenye ngazi ya Udiwani.

Mfano pale kata ya Mjimpya kikao cha Kamati ya Siasa kilivunjika baada ya wajumbe kukataa kumpa Alama B Mtia nia Abuu Shayo ambaye alihamia CCM siku ya mwisho ya kuchukua fomu na kuchukus fomu kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani kata hiyo na katika kura za Maoni alipata kura 13 akiwa nyuma ya Mtia nia Rashidi aliyepata kura 37.
Waajumbe wa Kamati ya Siasa wakapendekeza Rashid apate Alama B na Abuu apate Alama C lakini viongozi wa Kikao hicho wakiongozwa na Ummy, Hamisi Senkoro na Ludy Walipinga huku wakisema ni ‘Maelekezo kutoka Juu’ na ni lazima apewe alama C na Mvutano huo ukapelekea kikao kuvunjika bila muafaka kufikiwa.

Na huko Kata ya Mawenzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa amebwaga Manyanga na kuna taarifa kuwa kapeleka barua ya kujiuzulu kwa katibu wa CCM Wilaya kutokana na Vitisho anavyopokea na kuambiwa afuate maelekezo kwa kushinikizwa kumuwekea Alama A mmoja wa watia nia ambaye ni wa upande wa Matajiri.

Huko wilayani Mnyukano bado umepamba moto kikao cha juzi Jumapili kilishindikana kuendelea baada ya Katibu wa CCM Wilaya kuibuka na Jina Moja tu na kusema ndio lijadiliwe la Kiongozi wa ‘CCM Matajiri’ ndugu Ibra Shayo na kuacha jina la Priscus Tarimo na kutokana na hili kikafanyika kikao cha cha dharura kilichoongozwa na Katibu wa Mkoa na kupendekeza majina yote yajadiliwe wao watajua jinsi ya kushughulika na jina la Priscus ili lisirudi linapoenda Kamati Kuu.

Wanachama wa CCM wanasema huu ni wakati Katibu Mkuu taifa atambue kuwa watendaji wake wanamuangusha na kusema malalamiko yapelekwe Ofisi za chama ni kusema umpelekee fisi akulindie kitoweo chako. Hao viongozi ndio wanaopanga hiyo mipango na ndio wanawaumiza wanachama.