Dar: Vigogo wa Total watiwa mbaroni

Makao Makuu ya Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania, mchana huu yamevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni maofisa wa Serikali na kuondoka na baadhi maofisa wake.

Taarifa zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa maofisa hao huenda wanatoka moja ya taasisi nyeti za Serikali.

Maofisa hao wameondoka na viongozi wanne wa Total wakiwa wamefungwa pingu na kupandishwa ndani ya magari mawili yaliyowasili ofisi hapo, eneo la Kurasini, Dar es Salaam.