Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameweka kambi Zanzibar ili kuongeza nguvu katika kampeni za ushindi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mzee Mwinyi, ambaye ni baba mzazi wa mgombea urais Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amepewa makazi jirani na eneo la kupanga mikakati ya ushindi kwa mgombea huyo, Fumba. Timu binafsi ...
Taarifa tulizo nazo zinaonyesha Bwana Mkubwa anakulia timing tu, kuna mtu anaandaliwa kuishika nafasi yako wakati wowote baada ya Uchaguzi. Huyu ni naibu wako, Rodrick Mpogolo ambaye kina Polepole na Msigwa wanapambana kila uchao kuhakikisha anakuwa SG wa CCM na wewe ukachinjiwe baharini. Kimsingi, Polepole pia anaitamani nafasi yako. Huenda hujasoma alama za nyakati, sisi tunakudokeza mapema. Hiki ndo chanzo ...
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima amethibitika kugawa Sh. 20,000,000 kwa kila kata. Uchunguzi wetu umebaini kwamba mgombea huyo amekuwa akigawa kiasi hicho cha fedha kila anakopita kufanya kampeni. Jana katika Kata ya Msasani Kisiwani, Kinondoni, Gwajima akiwa katika kampeni alikutana na viongozi wa vikundi vya vijana vya ...
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), imepunguza kiasi cha malipo ya wasimamizi wakuu wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. NEC imepunguza zaidi ya Sh. 100,000 mwaka huu, ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, 2015. Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa mwaka huu, wasimamizi wakuu wa vituo watalipwa TSh. 105,000. Katika uchaguzi uliopita walilipwa TSh. 210,00. Jumla ya wasimamizi wakuu ...
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, jana amewaeleza baadhi ya viongozi waandamizi na makada wa chama hicho kuwa wastahimilivu na waache kulalamika kuhusu fedha za kujikimu wakati wa kampeni. Kumekuwepo na manung’uniko kwa makada wa chama hicho ambao wanazunguka maeneo mbalimbali kuomba kura kwa wagombea wa CCM, kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani. Dk. Bashiru anaelezwa kusema ...
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amewakutanisha maaskofu 71 wa makanisa ya “kiroho” jijini Dar es Salaam akiomba msaada wao ili ashinde ubunge. Maaskofu hao walikutana Alhamisi iliyopita katika hoteli ya Picolo, iliyoko Kawe jijini Dar es Salaam. Taarifa zinaeleza kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa kuomba viongozi hao wa kiimani kupitia makanisa yao kusaidia Gwajima ...
Timu ya kampeni ya mgombea Ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima imeanza kampeni za nyumba kwa nyumba, ikiomba samahani kwa niaba ya mgombea. Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa timu hiyo ya kampeni, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), juzi ilikuwa Kata ya Bunju, ikiongozwa na wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa. Katika kampeni hizo, timu hiyo imekuwa ...
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media Group (CMG), Joseph Kusaga anatuhumiwa kufuja fedha za kampuni, matumizi mabaya ya uongozi na dhuluma kwa wanahisa wengine, zikiwemo za marehemu baba yake. Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa Joseph, maarufu kwa jina la Joe, amekuwa akitumia fedha zinazopatikana kupitia Clouds FM, kuanzisha biashara binafsi, kukwapua mali, hasa nyumba na mashamba ambayo yalinunuliwa kwa fedha za ...
Vitengo vya Usalama katika baadhi nchi na taasisi za kimataifa, vimetuma watu wao kufuatilia kwa karibu mchakato mzima wa kampeni za Uchaguzi wa Tanzania. Vyanzo vyetu vinaeleza kuwa maofisa wa nchi na taasisi hizo tayari wako nchini wakichunguza mienendo ya viongozi wa vyama, hasa wagombea urais, wakati wa kampeni. Imebainika kuwa miongoni mwa maofisa hao ni mawakili kutoka Mahakama ya ...
Makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao majina yao hayakupitishwa kugombea ubunge, wamewasilisha barua kuomba sababu za kukatwa. Wawili kati ya hao watatu, licha ya kuongoza katika kura za maoni, majina yao yalikatwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), hivyo kuenguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho tawala kwenye uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba 28 l, mwaka huu, 2020. Taarifa ...