Update 2: Maalim Seif alazimishwa kurudi nyumbani. Vipigo vyaendelea kutembezwa

Vikosi vya Usalama visiwani Zanzibar sasa hivi vipo njiani kumrudisha Maalim Seif nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi mkali.

Sharti ni asitoke ndani, abaki nyumbani kwake.

Wakati huohuo, vikosi vya usalama vinaendelea kutembeza vipigo kwa wananchi maeneo ya Mtendani visiwani Zanzibar kwa wafuasi wa upinzani ambao wanataka kupiga kura leo badala ya kesho.