Just In: Upigaji kura waanza usiku huu Zanzibar

Katika Jimbo la Pangawe, Shehia ya Kijitoupele, Unguja,  vijana wa CCM wameonekana wakisombwa na magari ya vyombo vya usalama kwa ajili ya kupiga kura za awali usiku huu.

Vijana takribani 15 wameingia katika kituo cha kupigia kura cha Tanwiri, wakiwa wamebeba maboksi ambayo yanaonekana kuwa na karatasi za kura ndani yake.

Magari ya Polisi ndiyo yamewashusha vijana hao na kuwasubiri kwa zaidi ya nusu saa na  baadaye kuondoka nao. Walisubiriwa kuanzia saa 3.21 hadi saa 3:57 usiku huu.