Mkakati: Lissu kukamatwa tena. Kufunguliwa mashtaka yasiyo na dhamana

Polisi wamerandaranda sehemu alipo Lissu ili wamkamate upya.

Taarifa kutoka chanzo cha uhakika zinadai makachero na Polisi wametanda kila sehemu wakisubiri atoke tu na kumtia mbaroni baada ya kubaini kuwa jana walikosea kumkamata eneo ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Kimataifa ni makosa.

Lissu akikamatwa, inasemekana atafunguliwa mashtaka ya uhaini (si ugaidi) na mkakati ni kuhakikisha anabaki kizuizini kwa muda usiopungua miaka 5.

Bado tunafuatilia kwa karibu kinachoendelea na tutakujuza wote walioshiriki katika kukamatwa kwake na maagizo yalipotoka.