Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), imepunguza kiasi cha malipo ya wasimamizi wakuu wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
NEC imepunguza zaidi ya Sh. 100,000 mwaka huu, ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, 2015.
Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa mwaka huu, wasimamizi wakuu wa vituo watalipwa TSh. 105,000. Katika uchaguzi uliopita walilipwa TSh. 210,00.
Jumla ya wasimamizi wakuu 80,155 watapokea fedha hizo kwa kazi ya siku moja; Siku ya kupiga kura – Oktoba 28, 2020.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, NEC imepanga kutumia Sh. Bilioni 330, ikiwa ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na gharama za Uchaguzi za mwaka 2015, ambapo Sh. Bilioni 180 zilitumika.
Gharama zote za uchaguzi wa mwaka huu zinabebwa na Serikali, ikiwa ni kodi za wananchi. Rais John Magufuli anatamba kwamba “kwa mara ya kwanza, Serikali inalipa kila kitu cha Uchaguzi kwa kodi za wananchi.”
Leave a Reply