Pamoja na kusema hadharani kwamba atawaruhusu wale waliomwandikia barua, lakini ukweli ni kwamba hakupenda wateule wake “waingie tamaa ya kutaka ubunge.” Wiki moja iliyopita tuliandika tukidokeza kwamba vigogo 13 walioandika barua kwa Katibu Mkuu Kiongozi wakiomba likizo bila malipo ili kutangaza kutia nia ya kuwania ubunge kupitia CCM watafyekwa. Baada ya habari hiyo baadhi ya vigogo hao walionekana Dodoma wakihaha ...

Huenda historia ya kuimarisha ndoa za wagombea urais Tanzania ikajirudia katika mchakato wa Uchaguzi mwaka huu, 2020. Ilikuwa ni Benjamin William Mkapa ambaye ndoa yake na Anne Mkapa iliyokuwa na mushkeli kwa muda mrefu, ilipoimarishwa mwaka 1995 baada ya mume kuteuliwa na CCM kuwa mgombea urais. Baada ya ushawishi wa marafiki kushindikana, viongozi wengine wakiwamo wastaafu walimshauri na kumuomba Anne ...

Heshima, hadhi na uaminifu kwa Vyombo vya Habari, hasa magazeti kwa sasa inaelekea kukoma baada ya wamiliki, waandishi waandamizi na wahariri kuhamia kwenye siasa. Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, 2020 umedhihirisha hivyo baada ya Viongozi hao wa Vyombo vya Habari kukimbilia kuomba kuteuliwa na Vyama vya Siasa ili kugombea nafasi za ubunge. Kwa uhakika, mwanzoni mwa mwezi huu tuliandika kuhusu ...

Jumla ya watoto sita ni zao la uhusiano wa kimapenzi kati ya Viongozi wa juu wa CHADEMA na wabunge wa Viti Maalum wa chama hicho. Idadi hii ni ya katika kipindi cha Bunge lililopita chini ya Spika Ndugai. Uchunguzi wetu uliofanywa kwa muda mrefu umegundua kuwa watoto hao; wawili wavulana na wanne wasichana, walipatikana kutokana na uhusiano wa mapenzi uliosukumwa ...

2015 Nov 05: John Magufuli is sworn in as the fifth President of Tanzania. November: After the political opposition did not recognize the President of Zanzibar – who was also present at the constituent session of the parliament after the election was canceled there – police forces enter the parliament and forcibly remove members of the opposition. December:  President Magufuli ...

Upo mpango uliosukwa kumnyang’anya pasi ya kusafiria Tundu Lissu mara atakapotua Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, ametia nia kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi wa mwaka huu, 2020. Lissu kutua nchini Julai 28, 2020 Vyanzo vyetu vya uhakika vinabainisha kuwa Lissu awali alitarajiwa kutua jijini Dar mnamo Julai 25, ...

Dudley Mbowe, mtoto wa kiume wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman A. Mbowe amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospital ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuumia vibaya kichwani. Kijana huyo jana alifanyiwa operesheni ya kichwa na inaelezwa hali yake ni mbaya. Sababu za kulazwa kwa Dudley inaelezwa kuwa ni baada ya kuanguka na kukigonga kichwa chake ...

Watendaji wa serikali 13  walioandika barua za kuomba likizo bila malipo ili wapate nafasi ya kugombea ubunge, wamefutwa kazi jumla. Vigogo hao wamo Wakuu wa Wilaya, Mkoa, Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma, ambao ni wateule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu Katiba. Habari zinaeleza kuwa watendaji hao, hata baada ya kumsikiliza Rais John Magufuli ...

WATANZANIA wawili waliokwapua kifisadi zaidi ya Shilingi bilioni 74, fedha za wananchi, bado wanaonekana mitaani na kwamba “hawagusiki.” Taarifa za kiuchunguzi zinaeleza kuwa watu hao licha ya kuhojiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa zaidi ya mara tano (kila mmoja) hawawezi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa walifanya ufisadi huo kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo waliokuwa ndani ya ...

Kushuka kwa mapato ya mauzo ya gazeti la Mwananchi na kuzuiwa kwa matangazo mengi toka taasisi na mashirika ya umma na serikali kunaongeza uchungu katika mlolongo wa changamoto za ustawi wa gazeti hilo kwa sasa. Kwa muda mrefu sasa, gazeti hilo limekuwa likichechemea kiuchumi huku taarifa za ndani zikionyesha kuwa limeanza kuelemewa na madeni yanayotokana na gharama za uendeshaji, hasa ...