Mtoto wa Mbowe aanguka, alazwa ICU

Dudley Mbowe, mtoto wa kiume wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman A. Mbowe amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospital ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuumia vibaya kichwani.

Kijana huyo jana alifanyiwa operesheni ya kichwa na inaelezwa hali yake ni mbaya.

Sababu za kulazwa kwa Dudley inaelezwa kuwa ni baada ya kuanguka na kukigonga kichwa chake vibaya wakati akiwa Yatch Club, iliyoko Leopard’s Cove, Msasani Bay jijini Dar es Salaam.

Club hiyo ni sehemu ya starehe ambayo inaruhusu wanachama tu kuingia na kustarehe. Gharama ya kuwa mwanachama ni dola 500 (zaidi ya Sh milioni 1) inayolipwa kila mwaka. Kiasi hiki hakihusishi gharama za vinywaji, vyakula, boti za kifahari na huduma nyingine za kiwango cha kimataifa.

Hili linakuja ikiwa ni siku chache tangu Freeman Mbowe adaiwe kuumizwa na kuvunjwa mguu akiwa jijini Dodoma ambapo baadaye alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar.