Vodacom na sera ya ajira kwa wapenzi wa jinsia moja. Imeajiri 27 wa aina hiyo

Tanzania sasa inalazimishwa kuingia kwa kasi katika ile inayoitwa “dunia ya kisasa ya haki kwa kila mmoja” baada ya kampuni za wawekezaji wakubwa kulazimisha ajira kwa watu wenye jinsia tata (wale wanaofanya mapenzi ya jinsia moja) maarufu kuwa LGBT+.

LGBT+ ni kifupisho cha Lesbian (wasagaji), Gay (wasenge), Bisexual (wenye jinsia mbili), Transgender (mtu aliyebadili jinsia kwa upasuaji) na + ikiwakilisha “haki” sawa na wengine.

Miongoni mwa kampuni hizo ni kampuni ya mtandao wa mawasiliano, Vodacom ambayo imebainika kuwa na watumishi wenye utata wa jinsia 27. Wengi wao (21) wakipatikana Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Kitalu nambari 23, eneo la Ursino, Barabara ya Old Bagamoyo, Dar es Salaam.

Idadi hiyo inakaribia matakwa ya sera za Vodacom inayoeleza wazi kuwa – “Kwa  idadi yoyote itakayoajiriwa, lazima kuwepo na asilimia tano ya watu wenye jinsia tata.”  Hivi sasa Vodacom Tanzania imeajiri watumishi 594, wengi wao wakiwa Watanzania.

Pamoja na kwamba ni agizo la sera ya kampuni tanzu ya Vodacom Group, Afrika Kusini na kampuni yake mama ya  Vodafone ya Uingereza, kwa upande wa Tanzania haiwekwi wazi na wanaotambua hilo ni viongozi wa juu wa Kampuni hiyo yenye wateja takribani milioni 13 (13,000,0000) kati ya wananchi milioni 44 wanaotumia mawasiliano ya simu ambayo ni sawa na asilimia 33 ya watumiaji wote wa simu za mikononi kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini za hadi Desemba 2019.

Sera hii haiwekwi wazi

Vodacom Tanzania inahofia kuweka wazi sera hii kwa sababu mila, desturi na hata imani za watu haziruhusu “kulea” tabia zozote zinazohusiana na masuala ya uhusiano wa jinsia moja.

Vodacom Tanzania wamekuwa “wakivutana” na kampuni tanzu iliyoko Afrika Kusini inayotaka waajiriwa wake wote Tanzania kupewa mafunzo ya namna ya kuishi na kuwajali watu wenye jinsia tata kama ilivyo Afrika Kusini na mataifa mengine ambako Vodacom inafanya biashara.