Mwaka 2014 mchakato wa ujenzi Mradi wa Dege Eco Village uliopo eneo la Dege Beach Kigamboni (Dar es Salaam), ulikuwa wa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited.
Mkataba kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa Mwaka 2012 na kuanzisha Kampuni ya Hodhi ya “Hifadhi Builders” ambapo AHEL ilikuwa na 55% na NSSF ilikuwa na 45%.
Ndani ya Asilimia za AHEL, 20% ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na 35% alitakiwa kuweka fedha taslimu.
Mkandarasi Mkuu wa Mradi
Mkandarasi Mkuu wa Mradi ni Kampuni ya Mutluhan construction industry Co Ltd ya Uturuki, alikuwa kiongozi wa Wakandarasi na Taasisi nyingine kadhaa waliosimamia vitengo tofauti.
Mradi huo ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 na gharama za mradi zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani Milioni 653.4 zingetumika, ambazo kati yake ujenzi ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola 108,906,113 (Jumla Mradi ungegharimu Tsh. Trilioni 1.5).
Taarifa rasmi za Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuwa hadi Juni 2018, NSSF ilishailipa Kampuni ya Hifadhi Builders Dola 133,838,662.2 (Tsh. Bilioni 305.8) kama mchango wake kwenye ujenzi wa mradi huo wakati Kampuni ya Azimio ikitoa Dola 5,500,000 (Tsh. Bilioni 12.6).
Mradi kusimama
Mwaka 20216 mradi huo ambao ulipangwa kuwa na nyumba, hoteli, hospitali, maduka, maeneo ya mapumziko, shule, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa ulisimama.
Ni wakati huohuo, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilionesha kuna Ufisadi wa Tsh. Bilioni 179 katika mradi huo.
Malipo kwa Wakandarasi
Mkandarasi Mkuu Mutluhan Construction alikuwa kiongozi wa wanaodai fedha kutoka kwa Wamiliki wa Mradi.
Baada ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano kupita, mchakato wa mazungumzo ya kulipa Wakandarasi na Wadau walioshiriki kwa namna yoyote kuuwezesha mradi ukaanza kufanyika.
Makubaliano yakapitishwa waanze kulipwa kwa kuanza na Mkandarasi Mkuu.
Upigaji kwa malipo ya Wakandarasi
Mkandarasi Mkuu wakati akikabidhi Mradi hadi alipofikia, aliambatanisha madai ya fedha anazodai pamoja zile zinazodaiwa na taasisi nyingine zote zilizofanya kazi au kushiriki kwa namna yoyote katika Mradi.
Orodha ya wanaodai (iliyoachwa na Mkandarasi Mkuu)
Makampuni ya kigeni (Uturuki)
- UYUMSOFT (USD 175,509)
- ENTEGRE (USD 168,475)
- BDC (USD 97,500)
- KROMAN (USD 418,000)
- WORKERS (USD 518,610)
- HEDEF MEKANIK USD (53691)
- BILGEPANO (USD 63,549)
- NARIN MEKANIK (USD 90,372)
- ILHAMI DINCEL (USD 162,515)
- KUWEYTTURK BANK (USD 1,255,000)
Jumla ni USD 3,003,222
Walipwaji (Kampuni na Taasisi za Wazawa)
- Nayan Enterprises (USD 348,676)
- Maweni Limestone (USD 151,299)
- CBA Bank (USD 1,104,096)
- Cops Security (T) Limited (USD 45,540)
- Jubilee Insurance (USD 656,257)
- Dezo (USD 4,207,532) – Hii ni BLACKLISTED FIRM
- Cats-Net (USD 726)
- H.M.H.Gulamali (USD 363,636)
- Fountain Petroleum Ltd (USD 118,122)
- Asar Ltd (USD 9,203)
- Fasana General Auto Spares (USD 9,203)
- Mantrac (T) Ltd (USD 43,686)
- Mega Wood Craft Product Ltd (USD 11,318)
- Metrol Plastic Industries Ltd (USD 1,455)
- Metsec (T) Ltd (USD 22,001)
- Oilcom (T) Ltd (USD 21,561)
- Petrolube (T) Ltd (USD 39,340)
- Rift Vally Security Co. Ltd (USD 6,973)
- Supreme International Ltd (USD 25,273)
- Unity Computers Ltd (USD 649)
- Allied Transports Agent (USD 47,147)
- Azania Bank O.D (USD 123,200 + 155,682)
Jumla kuu ni USD 9,091,406
Mkandarasi alitoa maelekezo kuwa orodha ya Wanaodai ilikuwa pamoja na majina na akaunti na taarifa zote za malipo, akieleza kuwa anataka walipwe moja kwa moja (direct) bila kutumia kwake, kwa kuwa anaogopa kudaiwa baadaye.
Kuhusu Kampuni ya DEZO (inafichwa umiliki wake)
Malipo yaanza kufanyika
Baada ya kukamilika kwa mazungumzo, inadaiwa NSSF na washirika wake wakamlipa Mkandarasi fedha anazodai kwa kazi aliyoifanya hadi hatua aliyofikia.
Baada ya muda, NSSF wakaanza kulipa WADAU wengine (Waliotajwa hapo juu) waliokuwa wanadai wengi wao wakiwa wazawa.
Malipo yakaanza kufanyika kwa awamu (installment), yakitoka kila baada ya muda fulani lakini wahusika wanaodai wakawa hawalipwi wao moja kwa moja.
Inadaiwa NSSF walikuwa wakimlipa ‘dalali’ ili awalipe wanaodai licha ya kwanza Mkandarasi Mkuu aliacha ushauri akitaka wanaodai wote walipwe moja kwa moja kwenye akaunti zao.
Kilichotokea ni kuwa wanaotakiwa kulipwa hawafikishiwi malipo yao na wanaofikishiwa hawapati malipo kamili kwani “DALALI” anakula chake juu kwa juu.
Leave a Reply