Kushuka kwa mapato ya mauzo ya gazeti la Mwananchi na kuzuiwa kwa matangazo mengi toka taasisi na mashirika ya umma na serikali kunaongeza uchungu katika mlolongo wa changamoto za ustawi wa gazeti hilo kwa sasa. Kwa muda mrefu sasa, gazeti hilo limekuwa likichechemea kiuchumi huku taarifa za ndani zikionyesha kuwa limeanza kuelemewa na madeni yanayotokana na gharama za uendeshaji, hasa ...
Michango ya NSSF ya Deogratius Mwanyika, aliyekuwa Rais wa migodi ya Pangea, North Mara Exploration na Bulyanhulu, imelazimika kutumika kulipa sehemu ya fidia ya makubaliano maalum kwa Serikali baada ya kukiri kufanya makosa ya uhujumu uchumi. Fedha kiasi cha TSh bilioni 1, kilichotwa na kuingizwa kwenye akaunti ya maalum ya fedha za serikali inayosimamiwa na Hazina iliyoko Benki Kuu ya ...
Tanzania sasa inalazimishwa kuingia kwa kasi katika ile inayoitwa “dunia ya kisasa ya haki kwa kila mmoja” baada ya kampuni za wawekezaji wakubwa kulazimisha ajira kwa watu wenye jinsia tata (wale wanaofanya mapenzi ya jinsia moja) maarufu kuwa LGBT+. LGBT+ ni kifupisho cha Lesbian (wasagaji), Gay (wasenge), Bisexual (wenye jinsia mbili), Transgender (mtu aliyebadili jinsia kwa upasuaji) na + ikiwakilisha ...
Katika Mkakati wa kisiasa uliosukwa na chama tawala (CCM) kudhoofisha vyama vya upinzani Tanzania kwa ‘kununua’ wabunge, nusura hamahama hiyo imkumbe pia Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea. Chanzo chetu cha uhakika kinabainisha kuwa Kubenea ambaye alikuwa na mpango wa kukihama chama chake, kila kitu kilikamilika kwa kiwango kikubwa lakini alilazimika kubadili msimamo wake baada ya kifo cha mfanyabiashara tajiri, ...