Kosa moja la kiufundi linaloweza kufanywa na Kamati Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na kupelekea jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro ni kumpitisha mgombea ubunge aliyegushi shahada yake ya sheria.
Huyu ni Habib Mruma aliyeshika nafasi ya tatu ambaye Baraza la Seneti la chuo Kikuu Mzumbe katika mkutano wake wa 67 uliofanyika tarehe 25 Novemba 2016 liliamua avuliwe Shahada ya Sheria (LLB) aliyotunukiwa katika mahafali ya 12, mwaka 2013.
Uamuzi huo wa Seneti ulifikiwa baada ya uchunguzi kuthibitisha kwamba kada huyo wa CCM aligushi baadhi ya matokeo yake ya kitaaluma ambayo yalimuwezesha kutunukiwa shahada hiyo ambayo ilifutwa.
Hakuridhika na uamuzi huo na mwaka 2018 alifungua maombi namba 20/2018 Mahakama Kuu ya Tanzania akiomba uamuzi huo wa Baraza la Seneti ufutwe kwa sababu tu Kamati ya Uchunguzi haikumpa haki ya kusikilizwa.
Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akakubaliana na kipengele hicho hivyo akaamua kufuta mwenendo wote wa kikao kilichomfutia yake lakini akasema uamuzi wake huo hauzuii vyombo vya uchunguzi kumfungulia kesi ya jinai ya kugushi.
Katika sifa ambazo kada huyo alizieleza wakati akigombea ubunge jimbo la Mwanga ambako kulikuwa na wagombea zaidi ya 40, ni pamoja na kuwa yeye ana LLB na anatembea na hukumu ya Jaji Feleshi ambayo kimsingi haikumuondolea tuhuma za kugushi matokeo ya kitaaluma.
Kimsingi uamuzi wa Jaji Feleshi hautengui maamauzi ya Senate ya Chuo bali mahakama ilitamka kwamba hapakuwa na ushahidi kwamba utaratibu wa kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi ulifuatwa.
Taarifa kutoka Mwanga zinasema kutokana na ukwasi wa fedha alio nao na rushwa aliyomwaga kwa baadhi ya viongozi wa CCM Mwanga, kada huyo anapambana kuhakikisha jina lake ndilo linalorudishwa kugombea.
Tunaelezwa viongozi wa CCM Mwanga ni kama wamechanganyikiwa kiasi kwamba walikiuka kanuni mbalimbali za Uchaguzi na hata wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya kumaliza kikao wao walijifungia ofisini na kugushi muhtasari.
Wakati wanachama wa CCM Mwanga wakisubiri Halmashauri Kuu ifanye uteuzi wa mwanachama atakayepeperusha bendera yake, Bwana Mruma kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wana harakati nyingi ikiwamo kutunga na kuzusha tuhuma kwa wagombea wenzake ili waenguliwe.
Ila kiuhalisia, yeye ndio hasa alitembeza rushwa na bado anaendelea kumwaga kwa viongozi wake ili wafanye juu chini kuhakikisha aliyeshika nafasi ya kwanza Joseph Tadayo na wa pili, Profesa Jumanne Maghembe hakuna anayerudi.
Lakini taarifa zinasema mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Henry Kilewo anasali usiku na mchana ili jina la Mruma lirudishwe apate sababu ya kuweka pingamizi kuwa mgombea huyo anatumia cheti cha kugushi.
Leave a Reply