Jumla ya watoto sita ni zao la uhusiano wa kimapenzi kati ya Viongozi wa juu wa CHADEMA na wabunge wa Viti Maalum wa chama hicho. Idadi hii ni ya katika kipindi cha Bunge lililopita chini ya Spika Ndugai.
Uchunguzi wetu uliofanywa kwa muda mrefu umegundua kuwa watoto hao; wawili wavulana na wanne wasichana, walipatikana kutokana na uhusiano wa mapenzi uliosukumwa na ushawishi wa ubunge wa Viti Maalum.
Watoto wawili miongoni mwa watoto hao walipatikana ndani ya mwaka wa kwanza wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililoongozwa na Spika Job Ndugai kwa mwaka 2015/16.
Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa watoto wengine walipatikana ndani ya uhai wa Bunge hilo kuanzia 2016 hadi Juni 16, 2020 lilipovunjwa.
CHADEMA walikuwa na wabunge wa Viti Maalum 37 (wanawake) na watoto hao ni sawa na asilimia 16.2 ya wabunge wote wa Viti Maalum wa chama hicho.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wabunge wengi wa Viti Maalum wamekuwa wakipata nafasi hizo kwa uendeleo hasa unaotokana na uhusiano wa Viongozi wa juu wa vyama vya siasa kikiwamo chama tawala CCM.
Kwa upande wa CHADEMA, wabunge wa Viti Maalum, hasa wale wenye miaka 27 hadi 35, kipindi wameingia bungeni walikuwa na uhusiano huo na vigogo wa juu wa chama hicho au wafadhili ambao mara nyingi wamekuwa hawapendi kujulikana sana kwa umma.
Miongoni mwa viongozi hao ni baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu, Wabunge na hata viongozi wengine, hasa wenye ushawishi mkubwa walio Makao Makuu ya chama hicho, Ufipa jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa vigogo hao wa CHADEMA, mmoja wao amezaa watoto wawili na kuamua kumhalalisha kimila mbunge huyo kuwa mke. Kiongozi huyo ana mke na Mkristo, hivyo haruhusiwi kufunga ndoa nyingine. Mwingine alifunga ndoa ya kiserikali na mbunge huyo, ingawa sasa wametengana.
Hivi karibuni Spika Ndugai alinukuliwa akisema wabunge wengi wa Viti Maalum wamekuwa wakipatikana kwa njia za hivyo, nyingine akidai zilikosa ustaarabu na utu. Pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo wa Bunge alilenga mazingira ya kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi ili kupatikana kwa nafasi hizo.
Majina ya watoto, mama na hata baba zao, kwa sasa hatutayaweka hadharani kwa kuwastahi wahusika.
Leave a Reply