Mtandao wa Wizi ndani ya Wizara ya Fedha

Tangu awamu ya pili iliyoongozwa na Mhe. Rais Mwinyi kumekuwa na wimbi kubwa la wizi wa fedha za umma either kupitia watumishi wa Umma au Taasisi mbalimbali. Hata hivyo katika kipindi chote hicho Serikali imekuwa ikiwanyooshea vidole watumishi wanaobainika kuhusika na wizi huo bila kuchunguzi hasa chanzo cha wizi huu.

Leo hii nataka kutoa taarifa ya kiuchunguzi kuhusu mtandao wa wizi wa fedha za Umma kutoka Wizara ya Fedha. Mtandao huu ulianzishwa Mwaka 1986 pale Wizara ya Fedha ukiwa na lengo na kuhakikisha wanamtandao wananufaika na fedha wanazozituma kwenye Taasisi mbalimbali kama ruzuku kwa matumizi ya ofisi hizo.

Mtandao huu upo Wizara ya Fedha na unaundwa na Idara tatu kama ifuatavyo;​

  • Idara ya Utawala​
  • Idara ya Bajeti​
  • Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali.​

Kwa mujibu wa uchunguzi, Idara hizi zinashirikiana katika kuratibu, kupanga, kutoa hela, kulipa na hatimaye kugawa mrejesho kutoka Taasisi zilizokuwa zimepewa hela. Kumbukuka sio kila mtumishi wa Idara anajua hili jambo ni wanamtandao tu ndio wanashirikishwa kwenye kuratibu na kufanikisha jambo hili kwa siri sana.

Idara ya Utawala ndiyo inaratibu wapi pa kupeleka, kiasi gani na nani wa kuzipokea fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuratibu mgao wa mrejesho wa fedha zote zilizorudi kuhakikisha kila mnufaika anapata anachostahili.

Baada ya mipango ya Idara ya Utawala kukamilika inapelekwa Idara ya Bajeti kwa ajili ya kuhakikisha fedha zinapatikana na kuzipeleka panapohusika. Wanachofanya Idara ya Bajeti ni kuongeza ruzuku mfano ya matumizi ya kawaida, au maendeleo kwenye Taasisi inayotumiwa hela.

Baada ya Idara ya Bajeti kukamilisha majukumu yao, fedha zinapokelewa na Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali ambayo inafanya malipo kwa kuwalenga wanamtandao nje ya Wizara ya Fedha ambao ndio watakaosimamia zoezi zima hadi kuhakikisha fedha zilizopelekwa zinarudi kinyumenyume kwa ajili mgao wa wanamtandao.

Uchunguzi unaonyesha mtandao huu ni mkubwa sana, kwani umeene kote nchini, kwenye Taasisi mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Wilaya, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, TAKUKURU, Taasisi mbalimbali,TAMISEMI, Waziri Mkuu, Bunge, Mahakama, Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais yenyewe.

Mtandao huu umejiimarisha kila kona kiasi kwamba kila mwanamtandao anapokamatwa na kupelekwa kwenye chombo chochote kuchukuliwa hatua anakutana na mwanachama mwenzao wa kumtetea. Ndio maana pamoja na kelele za siku nyingi za Serikali ikiwa ni pamoja na kuwakamata watumishi na kuwapeleka mahakamani lakini Serikali haijawahi kushinda hizo kesi hata ikitokea imeshinda inamchukulia hatua mtu ambaye hawezi kusababisha kumvunja kabisa huo mtandao kwasababu mtandao upo Wizara ya Fedha sio Halmashauri au Taasisi nyingine yoyote. Kwa kuthibithisha hili ni kwamba hakuna mtumishi wa Wizara ya Fedha aliyewahi kuunganishwa kwenye wizi huu. Kwahiyo, atakamatwa Mhasibu au Ejinia wa Halmashauri au Taasisi nyingine yoyote lakini aliwezesha hizo fedha zifike kule bado yuko ofisi.

Mtandao huu umekuwa ukiibuka na wakati mwingine ukinyweea kulingana na kiongozi aliyeko madarakani (Rais). Rais akiwa mkali sana na anachukua hatua haraka, huwa anauzoofisha mtandao huu, lakini Rais asipochukua hatua mtandao huu hushamili kwa kiwango cha juu sana.

KINACHOFANYIKA WANAPOTAKA KUIBA HELA
Kama uchunguzi ulivyotangulia kusema hapo juu, Idara ya Utawala ndio wanaratibu kiasi gani kinahitajika na nani au Taasisi gani itapelekewa na mwakilishi wao ni nani kwenye hiyo Taasisi zinakopelekwa hizo fedha atashughulikia mchakato wa kusimamia hizo fedha kuhakikisha zinarudi kwa wahusika ili waweze kugawana.

Mifano halisi ni hii;
Kwanza; Serikali ina utaratibu wa kukamilisha matumizi ya fedha zilizopangwa ifikapo Juni 30, kila mwaka. “Ikifika wakati huo, HAZINA wana uwezo wa kuichukua na ikabaki labda iwe imeandikwa barua ya kuombewa kibali maalum cha kuhamisha fedha kwenda mwaka unaofuata.” “Hapa Bunda mnatumia mwanya huo, kuziombea kibali. Kisha zinahamishiwa kwenye akaunti jumuifu ya amana, halafu zinatolewa na kutumiwa kinyume na utaratibu.” Amesema mchezo huo unafanywa na watu wachache kwenye Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu wa kitengo cha akaunti jumuifu ya amana kilichopo OR-TAMISEMI na hata Katibu Mkuu hawezi kujua mchezo huo wala Madiwani pia hawawezi kujua. “Mara nyingi wanaocheza mchezo huo hapa Bunda, ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Mweka Hazina na Mkurugenzi wa Mipango wa Halmashauri. Kwa mfano, mwaka wa fedha 2021/2022 waliomba kibali cha kuhamisha sh. milioni 871.4 ili ziweze kutumika baada ya muda. Lakini walihamisha sh. milioni 962 na kuzihifadhi huko.”

“Mbali na hizo, kupitia mawasiliano baina ya hawa watatu na wenzao wa TAMISEMI, zikaingizwa tena sh. milioni 215.3. Je, ninyi Waheshimiwa Madiwani mliziomba hizo fedha? Je mlijulishwa kwamba kuna fedha za ziada zimeombwa?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa hapana na madiwani waliokuwepo. Waziri Mkuu amesema kibaya zaidi, fedha hizo zinapotoka, zinaelekezwa kwenye kazi ambazo tayari zilishatengewa vifungu na ambazo tayari ziliombewa kibali. “Walitoa fedha na kuandika zimetumika kwenye jengo la utawala, kutengeneza fedha za hesabu za mwaka, jengo la wagonjwa wa dharura, posho ya kujikimu ya walimu wapya wa shule za msingi. Hizi zote zilikuwa na fedha zake, Je, zimeenda wapi?” “Kamanda wa TAKUKURU, nataka ufuatilie ni nani aliomba hizo sh. milioni 215.3? Ni kwa nini fedha hizi zitumike kwenye kazi ambazo tayari zina mafungu yake? Je, ni kweli hawa walimu walilipwa hizo posho? Kwa nini madiwani hawakujulishwa kuhusu mchakato wa fedha hizi?”

Hivi ndivyo mchakato unavyofanyika hadi kukamilika baada ya hapo fedha zinarudishwa kwa ajili ya mgao kwa wanamtandao.

Pili; MKURUGENZI ALIYETENGULIWA NA RAIS SAMIA NI MIONGONI MWA WANAMTANDAO WA WIZI TAMISEMI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana ametengua uteuzi wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Sumbawanga Bi. Catherine Mashalla. Mkurugenzi huyu aliyekuwa afisa elimu wilaya ya Kigamboni wakati wa serikali ya Magufuli kabla ya kupewa ukurugenzi huko Mpimbwe anatuhumiwa kukwapua fedha za umma shilingi bilioni 1.2 za kitanzania na wenzake 13. Huu ni mtandao mkubwa sana ambao sisi Kigogo Media tumekuwa tunasema upo ndani ya wizara ya fedha na TAMISEMI. Wizi wa fedha za miradi ya watanzania ni mkubwa sana na mtandao wake umeota mizizi mirefu sana na kuhusisha mawaziri na viongozi wakubwa serikalini na hawa akina Catherine Mashalla ni sehemu ndogo tu ya kundi kubwa lililoko nyuma ya wizi huu wa kimkakati.

WAZIRI MCHENGERWA UNAHUSIKA KWENYE HILI AU WEWE NI MZEMBE !! WIZI ndani ya serikali hasa TAMISEMI kimeekuwa ni kitu cha kawaida sana na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kiasi kwamba sasa imefika mahali kwa akili za kawaida tu ni rahisi kuwaza pengine haya ni kwa sababu ya uhusika wa waziri mwenye dhamana pale TAMISEMI au uzembe na hutokujali. Hatuwezi kuchukulia jambo hili kuwa la kawaida pale kila siku tunapoona kuna watumishi wa serikali hasa TAMISEMI wanapokwapua hela za maendeleo za wananchi kwa manufaa yao halafu sisi hatuna habari kama watanzania na vilevile waziri na manaibu wake hawana habari kabisa na hawajali yaani. Wizi unafanyika kwenye halmashauri nchini unaacha maswali mengi sana hasa kwa waziri Mchengerwa! Je?

Mchengerwa huyu kama waziri mwenye dhamana; 1. Anafanya nini hasa ofisini na haya yanatokea hana habari? Ni uzembe? Dharau? Kutokujali? 2.Kashindwa kusimamia hizi halmashauri? Wasaidizi wake kwa maana ya manaibu wanajielewa kweli? 3. Hajui mambo mengi sana yanayotokea huko mikoani kwenye hizi halmashauri? 4.Ripoti za CAG huwa anazisoma? na kama anasoma na kuzielewa au anaona hazina maana? HAYA maswali yanakuja kwa kuwa ndani ya TAMISEMI – DODOMA ilipo ofisi ya Waziri Mchengerwa kuna genge la majizi na yeye anajua lakini hana habari na anadharau na haoni kama hili ni tatizo lake kabisa. Kitengo cha kuratibu ,kupokea na kugawa fedha za maendeleo kwenye halmashauri zote nchini pale TAMISEMI kina watu wafuatao na waziri Mchengerwa anawajua;

1. Aidana Zabron Mponzi 2.Tumsifu Christopher Kachira 3.Adola Mwombeki Mbalilaki Watu hata ndiyo wanaopokea fedha za maendeleo kutoka HAZINA na kuzigawa kwenye halmashauri zote nchini kama ambavyo imepangwa na serikali lakini watu hawa wanashirikiana na wakurugenzi na mabwana fedha kwenye halmashauri kukwapua hela hizi na hakuna kitu wanafanywa. Waziri Mchengerwa inakuwaje hujui kuwa watu hawa wameshiriki kukwapua hela za maendeleo mabilioni ya shilingi kwenye halmashauri zifuatazo nchini ambazo ni Kigoma,Bunda,Butiama,Tarime,Serengeti,Mbogwe,Kigamboni na Muleba? Kama sisi tu raia wa kawaida tunajua wewe waziri unashindwaje kujua? JIBU ni jepesi kuwa unajua na umeamua kukaa kimya kwa kuwa unajua au huenda wewe unashiriki hii michezo. Kwa sababu kwa hali ya kawaida kuwezi kuacha watu hawa wakaendelea kuwa ndani ya serikali au wizara yako wakati unajua haya yote. Tunajua watu hawa wameshiriki kwenye matukio nchi nzima lakini wanalindwa kwa nini? Tunajua wanasafirisha fedha hizi kwenye magunia kuzipeleka Dodoma kugawana lakini nani anawatuma na kuwalinda watu hawa? Na mbaya zaidi ukitaka kujua kundi hili ni mtandao hatari unaohusishwa mawaziri na watu wazito serikalini wanawatishia wajumbe wa kamati waliozunguka kufanya uchunguzi juu ya suala hili kwenye hizi halmashauri na kuwahoji na kuwauliza wanafanya uchunguzi kwa kibali cha nani? Rais amewapa kibali cha kufanya uchunguzi wa huu wizi? Yaani inasikitisha sana kuona majitu yamepewa dhamana ya kumsaidia Rais kuongoza nchi halafu bado yanatetea wezi.

Hivi kukamata akina Adola na Mponzi kwa wizi wanaoufanya wanahitaji ruhusa ya Rais? Yaani kivipi? Kitendo cha kamati ya kuchunguza wizi huu na mtandao huu wa wizi ndani ya TAMISEMI kutishiwa na kuogopeshwa ni dalili ya wazi kuwa huu mtandao unawahusu watu wengi sana wakiwemo mawaziri na hawa akina Adola na Mponzi wanatumiaka tu kurahisisha mambo lakini kuna wahusika wakuu wa huu wizi wako TAMISEMI NA HAZINA. SERIKALI yetu ina mawaziri vijana wengi sana ambao kwa mtazamo wa kawaida tulidhani watasaidia sana kuleta maendeleo ya nchi hii,lakini tuna mawaziri vijana waliojaa tamaa ,ulafi na wanaowaza kukwapua kila hela ya maendeleo ya watanzania,wamejaa kupigana majungu na kutengenezeana ajali za kisiasa kila kukicha mpaka inafika mahali tunadhani vijana hawana mchango mkubwa kwenye kuwa mawaziri na kusaidia nchi hii.

Kwa sababu małengo yao ni tofauti na yale ambayo mamlaka za uteuzi zinakuwa zinadhani wameteuliwa kusaidia watanzania. Ifike mahali 2025 hakuna haja ya kuwa na mawaziri vijana kwa sababu hawana mchango wowote zaidi ya kufanya wizi na kutengenezeana majungu kila kukicha. Hivi karibuni tutapokea ripoti ya CAG na haya mauzauza lazima yawepo na kwa aina ya ufanyaji kazi wa Waziri Mchengerwa atadharau na mambo yatakwenda kwa kawaida. Yaani watanzania wataongea watasahau maisha na akina Adola na Mponzi yataendelea tu pale TAMISEMI.

Mtandao huu umekuwa ukijiimarisha mwaka hadi mwaka lakini bahati mbaya Serikali inashughulika na wanaokamatwa na Ngozi, hawahangaikii kufuatilia asili ya huu mtandao unatoka wapi na kuchukua hatua. Huu mtandao upo pale Wizarani na baadhi ya hao wanaokamatwa wakibanwa wanasema wao ni watekelezaji tu wa maagizo kutoka juu.

USHAURI KWA SERIKALI

Ili kukabiliana na mtandao huu ambao umejiimarisha sana na unazidiki kukua kila mwaka, uchunguzi wa kina ufanyike kwenye Idara hizo tatu na nyingine kama zipo maana mtandao unazidi kuongeza wanachama. Kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta wachunguzi wa kimataifa ili wafanye ukaguzi wa kina kuhusu fedha zote zinazotolewa pale Wizara ya fedha, zinaenda wapi kwa kazi gani na kwa kibali gani.

Nimesema wachunguzi wa Kimataifa kwasabubu Serikali ikimpeleka CAG pale hawezi kugundua kitu kwasababu naye Ofisi yake imo ndani ya huu mtandao, sasa haijulikani ni mtumishi gani ndani ya Ofisi yake ni mwanamtadao.

Uchunguzi huu uwe wa miaka mitano au zaidi, hapa ndipo Serikali itaweza kugudua hasa hasara ambayo Serikali inaingia kupitia mtandao huu.

Serikali ishughulikie chanzo cha fedha zinapotoka yaani Wizara ya Fedha ikiwa ni pamoja na kuusambaratisha kabisa huu mtandao. Huu mtandao ni mkubwa sana kiasi kwamba hauwezi kuvunjwa kiurahisi inahitajika uthubutu.

Kitu cha kushangaza ni kumsikia Waziri wa Fedha (Mwanamtandao) anavyojinasibu kuwa hakuna wizi wa fedha za Umma, ili hali akijua fika kwamba kuna mtandao Wizarani kwake. Hata hivyo, si kitu cha kushangaza kwasbabu anatimiza majukumu yake ya kuhakikisha mtandao huu unalindwa na kila mwanachama.

Kwahiyo yeye akiwa kama mwanamtandao anawajibika kuulinda mtandao wa wizi Wizarani kwake kwa nguvu zote.

Lakini ni jukumu la Serikali na wananchi kuamua kusuka au kunyoa, nje ya hapo huu mtandao ukiendelea kukua itafikia wakati utakuwa na uwezo wa kumuweka hata Rais madarakani kwa kuhonga mchakato wote wa Urais.