Siasa za Tanzania katika jicho la tatu: Nini kinaendelea?

  1. Mkuu wa Nchi anafariki akiwa madarakani… Huyu ndio Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa hili. Sasa anafariki akiwa madarakani. Hiki kiti ndio cha juu zaidi kwenye kila nchi. Hiki kiti ndio nchi yenyewe. Yaani Rais ndio nchi yenyewe (Usiopumbazwe na protokali za kisiasa).
  2. Katibu Mkuu Kiongozi anaaga Dunia akiwa kwenye kiti chake. Kwa wasiofahamu, huu wadhifa ni mkubwa sana kwenye utawala wa nchi, hata Waziri Mkuu ni mdogo kwa kiti hiki. Naweza kusema hata Makamu wa Rais ni mdogo kwa umuhimu wa kiti hiki kwa Rais. Huyu ni Rais mwenyewe kwa sura nyingine. Huyu ni mshikaji mkubwa wa Rais wa kupika na kupakua (Usidanganywe na protokali unayoona machoni hali ni tofauti katika uhalisia).
  3. Waziri wa Katiba na Sheria anaaga Dunia akiwa kwenye kiti chake. Hiki kiti ni alama ya utamaduni na ustaarabu wa nchi katika kujitawala; sasa anafariki akiwa madarakani. Yaani huyu ni ustaarabu wa nchi katika kila eneo. Sasa, anafariki akiwa kwenye kiti chake.
  4. Waziri wa Ulinzi anafariki Dunia akiwa kwenye kiti chake. Hiki kiti ni alama ya utekelezaji na uimara wa majukumu ya kiulinzi ya nchi. Kwa maneno mengine, huyu ndio mbeba mikoba ya ulinzi kwa ajili ya Rais. Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi n.k. ni kama vitengo vya ulinzi tu, na Msimamizi wake mkubwa kwa niaba ya Rais ni Waziri wa Wizara hii.
  5. Waziri wa Afya na Naibu wake naona wanapuyanga na Corona. Leo wanasema ipo Kesho wanasema haipo na Corona inaendelea kuwadondosha raia makumi kwa mamia. Kwa maneno mengine ukuta wa Afya wa nchi una-shake mithili ya tetemeko kubwa.
  6. Hatujakaa sawa, mwanamke anakaa kwenye kiti cha ukuu wa nchi (usiniambie hii ni kawaida). Mwanamke mwenyewe anatoka kwenye Imani ya watu wasioamini ukuu katika mwanamke. Na kama haitoshi, mwanamke mwenyewe anatoka kwenye nchi ambayo ni ndogo kiushirika (Zanzibar) kulinganisha na mshirika mwenzie (Tanganyika). Sio kwamba hili haliwezi kutokea, la hasha ila hutokea kwa maandalizi mahsusi kabisa. Kinachotia fora zaidi mwanamke huyo anakaa kwenye kiti cha ukuu kwenye Jamii ya mfumo dume ulioshika hatamu.
  7. Unadhani yameisha? Sikia na hii: Mjenzi Mkuu wa madaraja na barabara wa nchi anaaga dunia akiwa kwenye kiti chake. Yaani ni sawa na kusema huyu ndio anajua ramani ya namna ya kuunganisha nchi yote. Sasa, bila hili wala lile anadondoka kwenye kiti na kuhitimisha safari yake.
  8. Kwa kuongezea nyama zaidi: Kiongozi Mkuu wa chama pinzani anatiwa jela. Yes, ana kesi kubwa ya ugaidi. Nini kinaendelea?
  9. Kwa kuendelea mbele zaidi japo muhimu: Hivi nani anaelewa chanzo cha msimamo wa Mbunge anayepingana na Serikali yake (Gwaji boy). Mnamkumbuka Catherine, kimaadili ile imekaaje? Lakini chama kipo kimyaaaaaa!
  10. Tufunge dimba: Mama kwenye kiti kila siku anaonekana kupoteza uungwaji mkono kwa wananchi. Nani haswa anaelewa sera ya Mama ama hata uelekeo wake ni upi haswa kwa sasa? Halafu vipi PM mbona makeke yake hayaonekani tena kama kipindi kile kabla ya Machi?

Kwa jicho la tatu, nabaki najiuliza: Je, kuna nini kinaenda kutokea kwenye ardhi na anga ya Taifa hili?

Ordinary minds wanadhani aaahhh mbona kawaida tu haya, yeah ni kawaida kwa uwezo wa ‘perspective’ yao lakini si kawaida kwa perspective ya extra ordinary minds kama mie na wengine.