Rodrick Mpogolo: Mrithi mtarajiwa wa Dkt. Bashiru nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM

Chanzo chetu cha uhakika kinabainisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Bara, Komredi Rodrick Mpogolo ndiye anatarajiwa kuwa mrithi wa Dkt. Bashiru Ally katika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM.

Disemba 13, 2016 Halmashauri Kuu ya CCM ilimteua Mpogolo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara akichukua nafasi ya Rajab Luhwavi aliyeteuliwa kuwa Balozi.

Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato na baadaye mshauri wa Rais masuala ya siasa.

Mpogolo anaaminiwa sana na Magufuli na inadaiwa ni mkakati wa Mangula na timu ya watu wake katika kuhakikisha Iringa na maeneo jirani yanaendelea kushika nafasi nyeti nchini.